Kimbisa awashukia wanaokailia habari

Mmoja wa waandishi wa Habari mkoani Dodoma Banda John akitekeleza majukumu yake ya kila siku.Picha na Robert Dagaa

Na John Banda, Dodoma

WAKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma na wa Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] wametakiwa kutokalia Habari maana siyo za kwao ni za wananchi.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Bunge la Africa mashariki na kati MHE. Adamu Kimbisa alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza la waandishi  na wadau wa habari liliofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu Capital miyuji Dodoma.

Kimbisa alisema watu hawatakiwi kukalia habari maana kwa kufanya hivyo ni kukiuka agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa mwaka jana kwenye Semina Elekezi aliyoitoa kwa watumishi wa serekali wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu wakuu na wakurugenzi.

Alisema kukataa kutoa habari ni kosa maana ni kuwanyima wananchi uhuru wao wa kupata habari kinyume na katiba ya jamuhuri ya muungano inayotoa uhuru wa kupata na kuzitoa.

‘’Mtu yeyote anakataa kutoa habari ana matatizo hataki kuongea na vyombo vya habari kutokana na uoga ili maovu yake yasije yakajulikana ndiyo maana mara nyingi wakiulizwa badala ya kujibu nao wanauliza eti na kakwambia kuna haja gani ya kumjua wakati habari ni za wananchi na viongozi wanatakiwa kutoa bila kujiumauma’’, alisema Kimbisa

Aidha Kimbisa aliwapongeza waandishi wa habari kwa kukusanyika pamoja kwenye bonanza hilo ambapo aliwataka kufanya hivyo mala kwa mala maana kwa kufanya hivyo wanapata sehemu ya kusemea matatizo yao maana nyingi wao wamekuwa wakiwasemea wengine huku ya kwao yakilala.

Awali akisoma Risala ya waandishi waliokusanyika pamoja kwenye Bonanza Hilo kwa nia ya kufanya sauti moja katika utendaji wa kazi za kiuandishi mkoani hapa Faraji Mwagoah alisema wakurugenzi wa Manispaa Robert Kitimbo na wa CDA Pascus Mulagili wamekuwa kikwazo katika utendaji wa kazi za kiuandishi.

Mwagoah alisema wakurugenzi hao wamekuwa kikwazo kwa kutoatoa ushirikiano kwa vyombo vya habari hasa wanapotakiwa kutoa fafanuzi mbalimbali na waandishi wanaokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment