Huyu ndie Changa aliyechezea kichapo na mgambo |
Hivi ndivyo alivyoumizwa chinga huyu
Alex Yona Machela ni mkazi wa Dodoma na pia ni mjasiliamali (chinga) alipigwa tarehe 6/03/2013 mda wa saa 11:25 barabara ya Saba (One Way) karibu na kitemba hoteli iliyoko Dodoma mjini.
Alikuwa
anafanya biashara ya kuuza viatu. Sababu za kumpiga Chinga huyo ni kwa
sababu sehemu ambayo alikuwa anafanyia biashara sio sahihi.
Alipakiwa kwenye gari la manicipal ya Dodoma akiwa salama ila alipofikishwa ndani ya ofisi ya Manicipal maasikari walianza kumpiga Alex (Chinga) kwa kutumia vitako vya bunduki na pia walimpiga kwa kutumia singa (ncha ya bunduki kwa mbele) maeneo ta mguu wake na kuumia vibaya.
Pia walitumia rungu kumpiga Alex kwenye miguu, mgongoni na mikononi bila huruma hii yote ni kwa sababu ya kuuza viatu sehemu ambayo sio sahihi hapa kweli kuna haki maana kama kweli amekosa ila sio kumpiga kama kibaka au mwizi kwa hali kama hii polisi watasababisha kutoelewana kati ya raia wema na wao maana hawana hata huruma kwa binadamu mwenzao na isitoshe ni mtanzania mwenzao.
Pia Alex (Chinga) alikuwa na viatu pear/ pics 120 ambazo mpaka sasa ziko Manicipal ya Dodoma na pia Manicipal walifungua kesi kwa kudai kuwa Alex Yona Machela alikwenda kumtetea muuza viatu ambaye alikuwa anauza viatu eneo ambalo sio sahii ndipo maasikari walianza kumpiga kwani alikuwa anawazuia wasifanye kazi yao.Kesi hii imefunguliwa mahakama ya mwanzo ya Chamwino iliyoko Dodoma mjini.
Kwa maelezo ya Alex (Chinga) anasema baada ya kushikwa kwa kuuza viatu sehemu ambayo hairuhusiwi alipandishwa kwenye gari akiwa na pear zake 120 za viatu ambazo maasikari walizishika wakaelekea municipal ya mji wa Dodoma lakini baada ya kufikishwa ofisini maasikari walianza kumshushia kipigo kwa kusema hii ni fundisho kwa wengine.
Anaendelea kusema alipigwa mpaka akapoteza fahamu.
Na
pia anasema kesi aliyofunguliwa na Manicipal sio ya kweli kwani viatu
ni vya kwake na wali sio vya mtu mwingine kama manicipal wanavyodai
kwani wanataka kujikinga kwa kusema uhongo ili kupoteza ukweli wa jambo
na mali yake ipotee kwa kutumia mgongo wa mahakama.
No comments:
Post a Comment