Abiria
mmoja raia wa nchini China, ambaye jina lake halikufahamika mara moja
ambaye amevunjika mguu wa kushoto akipewa huduma za matibabu mara baada
ya ajali ya basi la Green star lililogonga lori la mbao katika eneo la
kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya majeruhi wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa wa Singida,wakisubiri kupata matibabu.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Singida,wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya
mkoa,kuwaona majeruhi wa ajali ya basi la Green star iliyotokea jana
(10/3/2013) katika kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.(Picha na Nathaniel
Limu).
Watu
watatu wamefariki dunia baada ya basi T.939 BRA aina ya Yutong,
lililokuwa likitokea Dar-es-salaam likielekea Kahama mkoani Shinyanga,
kugonga kwa nyuma lori T.268 CCC likivuta tela T.931 CBU aina ya
Scania.
Watu
hao waliofariki kwenye ajali hiyo ni dereva wa basi hilo Yassin
Ramadhani (39) na msaidizi wake (utingo) Mansory Mohamed (30).
Wafanyakazi hao wa basi hilo wamefariki wakiwa wanapatiwa matibabu kwenye maabara ya hospitali ya mkoa mjini Singida.
Mwingine
aliyefariki kwenye ajali hiyo ni mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na
miaka mitano ambaye alifariki papo hapo kwenye eneo la tukio, hata
hivyo,jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa alimesema ajali hiyo imetokea
katika kijiji cha Nkuhi tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi katika
barabara kuu ya Dodoma – Mwanza.
Amesema
pia katika ajali hiyo, jumla ya abiria 20 wakiwemo raia watano kutoka
China na Uganda, walijeruhiwa na wamelazwa katika hospitali ya mkoaya
mjini Singida wakipatiwa matibabu.
Sinzumwa
ametaja raia kutoka China waliojeruhiwa ni Pisha Leng (45) amevunjika
mguu wa kushoto, Changshing Chang (43) na Guongrung Gang na wote
wanafanya kazi katika kampuni ya CCCC iliyopo Nzega mkoani Tabora.
Ametaja
raia wengine kutoka Uganda kuwa ni Swahibu Semgenyi (50) amevunjika
mguu wa kulia, Everine Mbine (33) na Tusime Aneti (33) na wote ni walimu
kutoka chuo cha Uganda.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kutaka kulipita lori lambao ambalo lilikuwa mbele.
Kamanda
Sinzumwa ametumia fursa hiyo, kuwakumbusha madereva wa vyombo vya moto
kujenga utamaduni wakuchukua tahadhari wakati wote ili kupunguza
uwezekano wakutokea kwa ajali zinazosababisha vifo na uharibifu wa mali.
No comments:
Post a Comment