Na John Banda, Dodoma
WANANCHI wa
katongoji cha Njedengwa wamefurahishwa na hatua zilizochukuliwa na viongozi wa
juu wa serekali ngazi ya Wilaya baada ya kuingilia kati malalmiko
waliyoulalamikia uongozi wa kata kutoingilia kati Swala la kuitisha mkutano kitongojini
hapo.
Wananchi hao waliokuwa
wakidai kuitishwa kwa mkutano ili waweze kutoa kelo mbalimbali zinazowasumbua
kitongojini hapo walisema wamefurahishwa na hatua yaserekali kusikia kilio chao
na kuamuru mkutano uitishwe.
Mwenyekiti wa Uhamasishaji wa
madai hayo Khatibu Mayuni alisema kutokana na barua walioandikiwa viongozi wa
kata hiyo ya kutakiwa kuitisha mkutano mkuu wa kitongoji jumanne ijayo imewapa
faraja na kuona kumbe serekali inaweza kusikiliza kilio cha wananchi.
Mayunini aliongeza kuwa
kutokana na usumbufu waliokuwa wanaupata toka kwa viongozi hao wa kata walikuwa
wameadhimia kuomba kibali na kufanya maandamano mpaka bungeni ili wakatetewe na
wabunge waliowachagua kutokana na kukosa haki ya kuuliza wala kutoa maoni ya
mapato na matumizi.
‘’Mwanangu unadhani tungeweza
kutolea maoni yetu wapi
kama si katika mikutano ambayo viongozi
wamegoma
kuiitisha kwa kipindi cha miaka mitatu sasa
bora sasa
nadhani kitaeleweka kwa sababu hata
mkurugenzi atakuwepo ili
ajionee mwenyewe wananchi unavyotafunwa’’, alisema
Wakati huohuo Barua
iliyoandikwa na afsa utumishi wa Manispaa Lawrence Malangwa Kwa niaba ya
Mkurugenzi imemtaka afsa mtendaji wa kata hiyo Magreth Songolo kushiriki kuuandaa
na kuhudhuria mkutano huo ambao mkurugenzi
atasikiliza kelo za wananchi hao.
Barua hiyo Iliyoandikwa Tar
11 APR 213 yenye kichwa habari kuitisha Mkutano Mkuu wa Kitongoji cha njedengwa
na nakala zake kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa
Polisi Wilaya [OCD], Diwani wa kata hiyo na Mwenyekiti wa kitongoji cha
njedengwa ilisisitiza mkutano huo kufanyika Saa 9:30 alasili.
Kero za wananchi hao ni
pamoja na Kutoitishwa kwa mikutano kwa kipindi cha miaka mitatu,
Kutoshirikishwa Ugawaji wa viwanja 99 vilivyopimwa na CDA katika ugawaji,
kubinfsishwa kisima cha maji na zaidi ya nyumba 119 zilizobomolewa tangu
2010 ili kupisha muwekezaji huku wakiahidiwa kupewa eneo jingine la
makazi.
No comments:
Post a Comment