Moshi. Vipimo vya mgonjwa
aliyetoka nchini Senegal na kuwekwa kwenye karantini mjini Moshi kwa
tahadhari ya ebola, baada ya kukaa nchini kwa siku 14 vimepelekwa katika
maabara ya jijini Nairobi nchini Kenya kwa uchunguzi.
Mbali na vipimo hivyo, lakini madaktari na wauguzi
wote waliomhudumia na wanaendelea kumhudumia mgonjwa huyo, nao
wamewekwa kwenye karantini wakisubiri majibu ya vipimo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako wakati uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro
ulipokutana na wanahabari kutoa taarifa ya maendeleo na uchunguzi wa
awali.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa Kilimanjaro,
Leonidas Gama mbali na kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo, lakini alisema
maeneo yote aliyopita mgonjwa huyo tangu aingie nchini wameyabaini na
kuchukua tahadhari.
“Kwa kweli nampongeza sana mgonjwa mwenyewe ametoa
ushirikiano mkubwa sana. Hata magari aliyopanda akiwa hapa nchini
rekodi zake tumechukua ili kama ikitokea majibu yakaja tofauti tujue la
kufanya,” alisema.
No comments:
Post a Comment