Na Princess Asia
MISS Ilala inafanyika leo katika shoo
ambayo itasindikizwa na wasanii nguli wa miondoko ya Bongo Fleva, Chegge, Lady Jaydee,
Banana Zorro na Machozi Band, kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge uliopo
maeneo ya Namanga, Dar es Salaam.
Mratibu wa Miss Ilala 2012, Gadna G
Habash, ambaye kwa sasa ‘Kapteni wa Maskani la Times FM 100.5’, ameiambia BIN
ZUBEIRY jana kwamba katika shindano hilo, mshindi atajinyakulia Sh.
Milioni 1.5, wa pili Milioni 1, wa tatu 700,000 wa nne na wa tano 400,000 kila
mmoja na wengine wote watakaobaki, kila mmoja atapata Sh. 200,000.
Mbali ya wasanii hao, msanii wa luninga,
Steve Nyerere ndiye atakayeliongoza kama MC ambapo kesho watakuwa na Mkutano na
Waandishi wa Habari kwenye club ya City Sports Lounge kwa ajili ya kutangaza
zawadi.
Vimwana 14 wanaotarajiwa kupanda
jukwaani kuwania umalkia wa Kanda ya Manispaa ya Ilala, Redds Miss Ilala 2012,
kati yao 12 wiki iliyopita walishindana kwenye kategoria ya kipaji ambapo
watano kati yao walitinga hatua ya fainali, ambayo itamaliziwa siku ya shindano
lenyewe Ijumaa.
Katika kinyang’anyiro hicho mrembo Mary
Chizi alikuwa kivutio zaidi kwa jinsi alivyoonyesha umahiri wake wa wepesi wa
kujivingirisha mwili huku Mectilda Martin akizoa ukumbi mzima kwa kurap na huku
akiwa ameandana kwa kucheza hata mavazi yanayotumiwa na wasanii wa miondoko
hiyo.
Magdalena Munisi hakuwa nyuma kabisa
katika kumwigiza mwanamuziki nguli wa marekani, Ciara kwa umahiri wake wa
kulitumia jukwaa, lakini kubwa kuliko pia kwa mrembo Amina Sangawe alibuni nguo
kwa kutumia vipande viwili vya khanga ambapo aliliunganisha jukwaani kupitia
pini nakumvika mmrembo mwenzie.
Stella Moris kwa upande wake alionesha
ukali kwa kuimba.
Warembo hao, wamekuwa wakijifua kwa
takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss
Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na
Dickson Daudi wa THT katika shoo.
Miss Ilala, yenye rekodi ya kutoa
warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu),
2000 (Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na
Salha Israel anayeshikilia taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake
nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka
vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga na inadhaminiwa na City Sports
Lounge, Redd's Premmium Cold, Uhuru One, Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, gazeti
la Jambo Leo, 100.5 Times FM, Redio ya
watu 88.4 Cloud's FM.
Mbali ya walioingia tano bora katika
vipaji, warembo wengine wanaoshiriki shindano hilo ni pamoja na Mary Chizi,
Matilda Martin, Magdalena Munisi, Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella
Moris na Elizaberth Pertty. Wengine ni Wilmina
Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe, Noela
Michael na Phillios Lemi.
Mbali ya Redd's Premmiun Cold, wadhamini
wengine katika mashindano hayo ni pamoja na
Uhuru One, Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo,
Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na Amaya Salon.
|
Whitness Michael |
|
Amina Sangawe |
|
Magdalena Munisi |
|
Stella Morris |
|
Mektilda Martin |
|
Diana Simon |
|
Wilmina Mvungi |
|
Rehema Said |
|
Zawadi Mwambe |
|
Neema Mbuya; Mwalimu |
|
Sylvia Mashuda; Mwalimu |
|
Elizabeth Pertty |
|
Suzane Deodatus |
|
Mary Chizi |
No comments:
Post a Comment