Rais Obama aahidi kuisadia Burma zaidi
Obama ziarani Burma
Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuendelea kuunga mkono kwa dhati juhudi za kuleta mabadiliko nchini Burma.
Katika ziara yake fupi ya kihistoria, Obama
alikutana na Rais Thein Sein na kusema uamuzi wa mwisho kuhusu
kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Burma kutategemea jinsi taifa hilo
litakavyoshughulikia malalamishi yaliyokuwa yametolewa kuhusu ukiukaji
wa haki za binadamu.
Aidha Obama alikutana na mwanaharakati wa haki za kibinadamu na kiongozi wa upinzani, Aung San Suu Kyi.
Lakini alilaani mapigano ya hivi majuzi kati ya
Wasilimu na Wabudhist huko Burma magahribi, na akatoa wito wa
kujumuishwa kwa Warohingya, ambao ni Waisilamu, na ambao hawatambuliwi
kama raia.
No comments:
Post a Comment