JELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA.

Na Walter Mguluchuma-Blogs za Mikoa Tanzania
Mpanda

Mahakama  ya hakimu mkazi  ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi imemhukumu   Gaudensi John  (30)  maarufu  kwa jina  (sanya)  mkazi  wa Kata ya Usevya  Wilaya  ya Mlele  kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha

Hukumu hiyo  ilitolewa  hapo jana na Hakimu  mkazi mfawidhi   Chiganga Tengwa  wa mahakama ya hakimu  ya wilaya ya Mpanda baada ya kulidhika na  ushahidi ulio  tolewa  mahakamani na upande  wa mashitaka na  mshitakiwa

Awali mwendesha mashitaka  Razaro Masembo  aliiambia  mahakama kuwa mshitakiwa  alitenda kosa hilo  hapo Oktoba 8 mwaka jana majira ya saa 5 usiku

Siku hiyo ya tukio  mshitatakiwa  Gaudensi  alikwenda  nyumbani  kwa  Fedrick Yombason huku  akiwa  na  bunduki  aina ya gobole  aliyo itumia  kwenye tukio hilo

Masembo  alieleza mahakamani hapo  baada ya mshitakiwa  kuingia  ndani ya nyumba  ya Fdrick  alimtaka  ampatie  pesa  vinginevyo   kama hampi  pesa angemuuwa  kwa bunduki  hiyo ya gobole

Alisema mshitakiwa  baada ya kutumia  vitisho  kwa kutumia bunduki alifanikiwa  kupola  kwa Fedrick  kiasi  cha shilingi 1,700 000 na kisha alitokomea kusiko julikana

Hakimu Chiganga baada ya  kusikiliza  maelezo  ya  mwenendo  mzima wa kesi kwa upande wa mashitaka na mshitakiwa alidhika   ushahidi  ulio tolewa mahakamani  na alieleza kuwa mahakama  imemuona mshitakiwa  kuwa na hati

Hivyo  mshitakiwa aliiomba mahakama  kwenye utetezi wake impunguzie adhabu  kutokana  na kuwa na umri  mdogo na kuna familia inamtegemea  ombi ambalo lilipingwa vikali na mwendesha mashitaka

Hakimu Chiganga baada ya kusikiliza ombi la mshitakiwa la kuomba kupunguziwa  adhabu aliiambia mahakama kuwa   mshitakiwa  ametiwa hatiani na  kulingana na kosa hilo mahakama imemhukumu   Gaudensi  kwenda jela kifungo cha miaka 30.

No comments:

Post a Comment