Watuhumiwa mauaji ya Padri Mushi wakamatwa

*Wadaiwa kusafiri kwa Jahazi kutoka Z’bar hadi Mombasa
 
*Wanaswa katika usafiri wa gari wakielekea mjini Nairobi

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi nchini wamewatia 

mbaroni vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika 

katika mauaji ya Padri Everist Mushi (55) wa Kanisa 

Katoliki mjini Zanzibar.

Watuhumiwa hao wamekamatwa mjini Nairobi, 

Kenya kutokana na ushirikiano wa Jeshi la Polisi la 

Tanzania na Polisi wa Kenya kwa mwamvuli wa 

Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (Interpol).

Habari za kuaminika kutoka Nairobi, Kenya 

zimesema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao 

yamehifadhiwa, walitiwa nguvuni juzi mjini humo 

walipowasili wakitokea Mombasa, mashariki mwa 

nchi hiyo.

Watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiingia katika 

maficho kukwepa mkono wa dola, wanadaiwa 

kutumia jahazi kusafiria kutoka Zanzibar hadi 

Mombasa, Kenya kabla ya kusafiri kwa magari hadi 

Nairobi ambako walitiwa nguvuni.


Habari na Jamii Forums.  kupitia ITV

No comments:

Post a Comment