Wachuuzi hao wakibeba moja ya kibanda cha
kufanyia Biashara zao wakati walipotangaziwa stendi hiyo iliyokuwa
Katika viwanja vya Nanenane Nzuguni kufungwa na Naibu Meya wa Manispaa
ya Dodoma Jumanne Ngede.
Na John Banda, Dodoma.
Wasukuma mkokoteni wakihamisha moja ya
vibanda vya wafanya biashara baada ya kutakiwa kuhama baada ya stend
hiyo iliyokuwa Viwanja vya nanenane Dodoma kufungwa kabla ya Ukarabati
unafanywa stand za Daladala na ile ya mabasi yaendayo mikoani kukamilika
Wafanyabiashara ndogo ndogo wakichimba
masimo ili waweze kurudishia vibanda vyao vilivyobomolewa na watu
wasiojilikana nyuma ya Baa ya Actik iliyopo stand ya Daladala jamatini
Dodoma
Machinga katika manispaa ya Dodoma
wakihamisha matofali yaliyopangwa nyuma ya uzio wa baa ya Actik iliyopo
jamatini ili waweze kujenga vibanda vyao vilivyobomolewa na watu
wasiojulikana baada ya kuondolewa zilipokuwa Stand za muda za Daladala
na za mabasi yaendayo mikoani Nanenane.
PICHA NA JOHN BANDA
WACHUUZI 96 waliokuwa katika Staendi ya
Daladala Jamatini manispaa ya Dodoma ambayo kwa sasa ipo katika ukarabati mkubwa wamemlalamikia
mfanyabiashara wa bar ya Actic iliyopo pembezoni mwa eneo hilo kwa kitendo
chake cha kuhamisha na kuvunja vibanda vya biashara zao bila utaratibu.
Wachuuzi hao maarufu kama machinga walisema
walijenga vibanda vyao tena mala baada ya kupewa maaelekezo ya kufanya hivyo na Mamraka ya Ustawishaji Makao Makuu [CDA] waliowambia
wakatafute maeneo ya kuweka vibanda hivyo na kisha waende kuwaambia ili
wakawathibitishe.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Stendi ya
Daladala Jamatini Haji Kulaya pamoja na baadhi ya wanachama wanaowakilisha
wenzao 96 walisema waliandika Barua CDA
wakaambiwa wakati majibu yanashuhulikiwa wao wakaendelee na ujenzi wa vibanda
vya muda katika eneo hilo wakati wanasubili ukarabati ukamilike.
Mwenyekiti Kulaya Alisema walipofika walikuta Miti yote waliyokuwa
wamechimba kwaajili ya kujenga vibanda walikuta imeng’olewa huku vibanda vikiwa
vimehamishwa na kuvunjwa vunjwa hovyo na walipotaka kujua waliambiwa Mwenye Bar
ndiye aliliyefanya uharibifu huo na wao wakaamua kwenda CDA kulala mika.
‘’Sikilizeni ndugu waandishi sisi tunaweka
vibanda hivi maana tokea tulivyoambiwa twende Nanenane Baada ya ujenzi tutarudi
Sasa Stendi hiyo imefungwa twendwe wapi wakati sisi tulikuwa hapa wenzetu wa
kwenye mabasi ya mikoani mbona wamerudishwa sisi tumerudi huyu tajiri ameanza
kutuvunjia au walituondoa ili eneo hili apewe yeye?’’, Alisema Kulaya
Mkurugenzi Wa Actik Bar Fredy Sam alikanusha
kuhusika na uvunjaji huo na kusema yeye baada ya kukuta vibanda vmejengwa
katika eneo lake la maegesho kwa ajili ya wateja wake akaamua kuwajulisha CDA
na ndiyo waliovunja yeye asihusishwe kwa kuwa yeye hana mamlaka.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamraka
ya Ustawishaji Makaomakuu [CDA] Ibrahimu Ngwade Alilema wao kama Mamraka
hawahusiki wenye majibu ni mkurugenzi wa manispaa kwani ndiyo anajua ni wapi wanapotakiwa
kuwekwa wachuuzi hao, lakini akaongeza
mtu yoyote awe hao wenye vibanda au huyo mwenye Bar wakivunja sheria lazima
watavunjiwa.
Nendeni kwa Mkurugenzi wa Manispaa Atawapa
majibu, sisi kama Mamraka tanatoa maeneo lakini mtu yeye akijenga zaidi ya
mpaka wake lazima avunjiwe kwa hilo hatujali hao wenye vibanda wala huyo mwenye
bar’’, alisema
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Nicolaus
Buleta alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo alisema hawezi kuzungumzia
jambo hilo kutokana na kuwashuhulikiwa na ofisi ya katibu tawala wa mkoa.
‘’Hilo siwezi kulizungumzia nendeni Ofisi ya
RAS ndiyo iliyokuwa inashuhulikia swala la Nanenane Wafanyabiashara, kwa sasa
niacheni naenda Hosipital Muhasibu wetu anaumwa amevimba tunataka kumpeleka
muhimbili Da es alaam’’, alisema Buleta
Mwanzoni Mwa mwezi Naibu Meya wa Manispaa
Jumanne Ngede alitangaza kuifunga Stendi hiyo ya Muda iliyokuwa Nzuguni Ndani
ya Viwanja Vya Nanenane kabla ya muda wa miezi 8 uliokuwa kwenye makubaliano
kufika huku akiwataka wafanyabiashara hao kufuata mabasi yatakapopakilia na
kushushia abiria bila kutoa maelekezo ni wapi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment