Papa Benedict XVI,
Vatican.Mchakato wa kumchagua Papa mpya wa
Kanisa Katoliki umepamba moto wakati misa maalumu ya kuandaa uchaguzi
huo ikifanyika katika makao makuu ya Kanisa la Mtakatifu Peter wa
Basilica lililopo Vatican.
Makardinali 115 wenye umri wa zaidi ya miaka
80 ambao wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo, watafungiwa ndani ya
hekalu la Sistine ambako zoezi zima litafanyika.
Papa Benedict wa 16
alijiuzulu mapema mwezi Februari na kuupa ulimwengu mshtuko baada ya
kuwa ni Papa wa kwanza kujiuzulu kwa kipindi cha miaka 600 iliyopita.
Katika hotuba yake ya mwisho, Kiongozi wa Chuo
Cha Makardinali, Kadinali Angelo Sodano alihimiza umoja ndani ya Kanisa
Katoliki na kuwaasa makadinali watakaopiga kura kuweka pembeni tofauti
zao kwa manufaa ya kanisa na kwa Papa wa Mpya.
“Kila mmoja wetu hapa anatakiwa kutoa
ushirikiano wake kwa mrithi wa Papa Benedict XVI, tudumishe umoja na
mshikamano” alisema Kardinali Sodano Hii ni kauli nzito ya mwisho
kutolewa na Kardinali wa Vatican kabla ya kuteuliwa kwa Papa mpya.
Hata hivyo Kardinali Sodano hatashiriki uchaguzi huu kwani ana umri wa zaidi ya miaka 80.
Kabla ya uchaguzi, makardinali wote wataapishwa kwa kula kiapo cha kutunza siri ya matukio yote wakati wa uchaguzi huo.
Aidha imeelezwa kuwa zoezi hilo linaweza
kudumu kwa siku kadhaa kwani makardinali hao huenda wakapiga kura zaidi
ya mara nne hadi pale mrithi wa Papa atakayeliongoza kanisa hilo lenye
waumini zaidi ya bilioni moja duniani atakapopatikana. Makardinali hao
watatakiwa kuanza mchakato mzima wa zoezi hilo saa 10.30 leo. Baada ya
kula kiapo maneno kama “extra omnes” na kila mmoja yatatamkwa.
Katika mchakato huo makardinali wataandika
jina la Papa wanayempendekeza katika kipande cha karatasi na kukirusha
katika chombo maalumu.
Watabiri wa mambo wanadai kuwa katika mchakato
huo huenda ukatokea uwezekano wa Papa mmoja kati ya makardinali 115
kupata kura 77 au robo tatu, na ndiye atayekuwa papa katika uchaguzi wa
kwanza.
Hata hivyo makardinali hao wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Papa mpya watakayemteua.
Kumekuwa na mawazo tofauti iwapo Papa mpya awe
anatoka nje ya Jiji la Vatican au chaguo kutoka ndani ya Vatican ili
alete mabadiliko kutoka ndani.
No comments:
Post a Comment