Tanzania yapeleka vipimo vya ebola Nairobi



Moshi. Vipimo vya mgonjwa aliyetoka nchini Senegal na kuwekwa kwenye karantini mjini Moshi kwa tahadhari ya ebola, baada ya kukaa nchini kwa siku 14 vimepelekwa katika maabara ya jijini  Nairobi nchini Kenya kwa uchunguzi.
Mbali na vipimo hivyo, lakini madaktari na wauguzi wote waliomhudumia na wanaendelea kumhudumia mgonjwa huyo, nao wamewekwa kwenye karantini wakisubiri majibu ya vipimo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako wakati uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro ulipokutana na wanahabari kutoa taarifa ya maendeleo na uchunguzi wa awali.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama mbali na kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo, lakini alisema maeneo yote aliyopita mgonjwa huyo tangu aingie nchini wameyabaini na kuchukua tahadhari.
“Kwa kweli nampongeza sana mgonjwa mwenyewe ametoa ushirikiano mkubwa sana. Hata magari aliyopanda akiwa hapa nchini rekodi zake tumechukua ili kama ikitokea majibu yakaja tofauti tujue la kufanya,” alisema.

No comments:

Post a Comment